Tuesday, September 10, 2013

FORMULA1 : Ferrari waibomoa Lotus,Alonso,Raikkonen timu ya hatari


Kimi Raikkonen yupo karibu kabisa kuthibitishwa kama dereva wa Ferrari kwa msimu wa mwakani wa Formula 1.

Kurejea huko Maranello kwa Raikkonen kunamfanya kuungana na timu iliyomfanya kuchukua taji la dunia 2007 na inaelezwa kuwa mpango wa kurejea umekamilika jana na kinachosubiriwa ni kutangazwa rasmi.

 
Raikkonen, 33,atakuwa timu moja na Fernando Alonso,bingwa wa 2005-6,na kuifanya kuwa timu imara kwenye Formula 1.

Maamuzi hayo yanaweza kumuondoa kwenye timu dereva raia wa Brazil Felipe Massa aliyedumu kwa miaka nane kwenye timu hiyo maamuzi yanayosubiri baraka za Rais wa Ferrari Luca Di Montezemolo.

Raikkonen alikuwa na chaguo la kubakia kwenye timu yake ya Lotus lakini timu hiyo imeshindwa kutekeleza matakwa yake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.