Wednesday, September 18, 2013

Iker Casillas anahitaji maombi,kama ni mganga wa Lopez kibokooo


Unaweza ukaanza kwa kusema golikipa namba moja wa Hispania aliyepoteza namba yako kwenye timu ya Real Madrid Iker Casillas anahitaji maombi baada ya kucheza kwa dakika 13 tu kwenye mchezo ambao alirejeshwa kunako kikosi cha kwanza katika mchezo wa ligi ya mabingwa kundi B dhidi ya Galatasaray uliomalizika kwa Madrid kupata ushindi mpana wa mabao 6-1.


Casillas baada ya kupoteza namba yake kwa golikipa Diego Lopez tokea enzi za Mourinho na hata kwa kocha mpya Carlo Ancelotti,jana alirejea langoni kwenye mchezo huo akiwa kipa chaguo la kwanza lakini ndani ya dakika 13 akiwa anadaka mpira akagongwa mbavu na mchezaji mwenzake  Sergio Ramos.
Licha ya kujilazimisha kutaka kuendelea kusimama langoni bila shaka akitaka kuendelea kumshawishi kocha amrejeshe langoni kupitia mchezo huo timu ya madaktari ilimfunga bendeji kuzunguka mbavu zake lakini ndani ya dakika moja akasalimu amri na kupiga mpira nje kuashiria amekubali yaishe na nafasi yake ikakamatwa na kipa anayetesa langoni kwasasa katika timu hiyo Diego Lopez.
Kocha Carlo Ancelotti amesema Casillas anaweza akawa vizuri na kurejea kwenye afya yake ndani ya siku tatu mpaka nne japo inaelezwa kuwa yawezekana kipa huyo mwenye miaka 32 akakaa nje kwa wiki mbili.

Mshambuliaji aliyetupia wavuni mabao matatu "hat-trick",Cristiano Ronaldo amesema kipa huyo ana bahati mbaya japo hayo ni mambo ambayo hutokea kwenye soka.

Itakumbukwa Casillas amekua akisugua benchi kwa muda mrefu na aliwahi pia kukumbwa na tukio la kuumizwa na kuvunjwa mfupa wa mkono na mchezaji mwenzake Alvaro Arbeloa mwezi January.

Kama ingekuwa bongo watu wangeanza kupiga kelele kuwa kipa huyo anapigwa misumari(anarogwa)na kipa mwenzake Lopez ambaye sasa anatawala langoni kama enzi za Mourinho ambapo katika msimu huu chini ya Ancelotti tayari amecheza mechi zote nne za ligi kuu ya Hispania wakati Casillas akisotea bench

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.