Wednesday, September 4, 2013
Spurs ilimbania Ozil kutua Arsenal,Madrid wakawasaliti
Mwenyekiti wa TOTTENHAM Daniel Levy alitaka Real Madrid waibanie Arsenal kwa Mesut Ozil na katika siku ya mwisho ya usajili akampigia simu Rais wa Madrid Florentino Perez akimshawishi kuipiga chini ofa ya Arsenal.
Levy aliamua kufanya hilo akitumia uhusiano wao uliojengeka baada ya kuwauzia kiungo Luka Modric ili kuwavunja nguvu Arsenal ambao ni wapinzani wao wakubwa kucheza Champions league.
Baada ya Ozil kukamilisha mpango wa kujiunga Arsenal,Levy anahisi amesalitiwa na Madrid ambao mwanzoni alitaka mpango wa kumuuza Gareth Bale na mchezaji huyo.
Lakini kwa wakati huo Perez alimwambia Levy kuwa Ozil hauzwi na ataendelea kubakia Santiago Bernabeu.
Habari hizo za Ozil kutua Arsenal zinaweza kuzorotesha uhusiano baina ya timu hizo mbili ikichangiwa pia na Levy kuchelewesha kukubali kuwauzia Madrid Gareth Bale.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.