Wednesday, September 11, 2013

KOMBE LA DUNIA 2014 : Uholanzi,Italy ndani


Timu ya taifa ya Uholanzi The Orange na Italy Azzuri zimekuwa nchi za kwanza barani Ulaya kukata tiketi ya fainali za kombe la dunia 2014.

Robin van Persie ametupia wavuni mabao mawili wakati waDutch wakiichapa Andorra 2-0, na Uturuki wakishinda mabao 2-0 mbele ya Romania kukaihakikishia Italy kuendelea kukaa kileleni mwa kundi D.

Italy ilikuwa ikihitaji ushindi mbele ya Czech Republic ili kufuzu na mabao kutoka kwa Giorgio Chiellini na Mario Balotelli yemetosha kuipeleka kwenye fainali hizo licha ya bao la Czech lililofungwa na Libor Kozak.

Belgium, Germany na Switzerland zinahitaji pointi mbili kila mmoja ili kufuzu kwa fainali hizo.

Germany angalau imejihakikishia hatua ya mtoano baada 7ya ushindi wake wa mabao 3-0 dhidi ya Faroe Islands mabao ya Per Mertesacker,Mesut Ozil na Thomas Muller.

Zilizofuzu

  • Brazil (hosts)
  • Japan
  • Australia
  • Iran
  • South Korea
  • The Netherlands
  • Italy

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.