Friday, September 20, 2013

FORMULA1 : Hamilton awakimbiza Singapore


 
Dereva wa Mercedes Lewis Hamilton amemaliza kwenye nafasi ya kwanza katika majaribio0 ya kwanza ya Singapore Grand Prix.

Hamilton amemuongoza dereva wa Red Bul Mark Webber kwa sekunde 0.365 huku nafasi ya tatu ikiangukia kwa Sebastian Vettel naye wa Red Bull.
 
Dereva wa pili wa Mercedes Nico Rosberg amemaliza nafasi ya nne akiwa nyuma kwa sekunde 1.184.

Dereva wa Lotus Kimi Raikkonen na Romain Grosjean wakafuatia kwenye nafasi ya tani na sita.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.