Gareth Bale anatarajiwa kufanyiwa vipimo leo baada ya kuumia muda mfupi kabla ya mchezo wa La liga uliochezwa jana huko Bernabeu.
Bale,ambaye ametua Real Madrid kwa dau lililoweka rekodi ya dunia la paundi milioni 85 ilikuwa ndio mchezo wake wa kwanza kucheza nyumbani tokea amesajiliwa.
Dakika moja kabla ya kuanza kwa mchezo huo dhidi ya Getafe ambao Madrid waliibuka na ushindi wa mabao 4-1 ililazimika nafasi yake acheze Isco.
Mkurugenzi wa Real Madrid Emilio Butragueno amesema mchezaji huyo alisikia maumivu sehemu ya paja na ikalazimika timu ya madaktari kumtazama na akabadilishwa na kuchezeshwa Isco kwenye nafasi hiyo.
Butragueno amesema maumivu aliyoyapata yanaonekana sio makubwa sana japo leo ndio watafahamu baada ya kufanyika vipimo.
Bale mchezo wake wa kwanza wa ligi alicheza dhidi ya Villareal uliomalizika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na yeye akitupia bao lake la kwanza tokea ametua kwenye timu hiyo.
Lakini pia itakumbukwa alicheza akitokea benchi kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Galatasaray ambao Real Madrid ilipata ushindi wa mabao 6-1.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.