Friday, September 20, 2013

England,Hispania,Wales,Ufaransa,Italy wataka uwenyeji wa Euro


England, Scotland, Wales na Jamhuri ya Ireland wameiambia Uefa kuwa wanataka kuwa wenyeji wa fainali za Ulaya 2020.

Uefa imesema wanachama wake 32 wameonesha nia baada ya kuwaambia kuwa maamuzi yaliyopita ni kwamba fainali za mwaka huo zitachezwa katika miji 13 katika nchi tofauti za barani Ulaya.

England wanataka kuwa wenyeji wa mechi hizo katika jiji la London wakati Scotland wamechagua mji wa Glasgow.

Wales nao wametumbukia wakitaka kutumia mji wa Cardiff, nao jamhuri ya Ireland wakichagua mji wa Dublin.
Mataifa makubwa katika soka barani Ulaya ikijumuisha Ufaransa, Germany, Italy, Uholanzi na Hispania zimeonesha nia za kutaka kuwa wenyeji wa mechi hizo.

Nchi hizo pia zinaruhusiwa kubadili mji waliouchagua awali na mwisho wa kupeleka majina ya miji ni April 25 mwakani.

FA ya England wenyewe wanataka kuwa wenyeji wa hatua ya nusu fainali na fainali wakitaka zipigwe kwenye dimba la Wembley au mechi za hatua ya makundi na hatua ya mtoano.

Rais wa Uefa Michel Platini alisema kuwa anaunga mkono fainali kuchezwa Istanbul kama Uturuki itapoteza uwenyeji wake wa michezao ya Olympic mwaka 2020.

Uefa itaamua September 25 2014 kuhusu miji hiyo 13 itakayokuwa wenyeji.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.