Friday, September 13, 2013

Ancelotti athibitisha kumuanzisha Bale kesho



Mchezaji ghali duniani Gareth Bale kesho ataanza kwenye kikosi cha kwanza kwa mara ya kwanza akiwa na Real Madrid kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Villarreal.

Kocha Carlo Ancelotti amethibitisha kumuanzisha mchezaji huyo raia wa Wales aliyeighalimu timu hiyo kitita cha paundi milioni 85.3 akitokea Spurs.
Bale hajacheza kwa dakika 90 tokea kuanza kwa msimu baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mguu na Jumanne iliyopita alicheza kwa dakika 32 akiitumikia timu ya Taifa ya Wales dhidi ya Serbia.

Swali kubwa ambalo wengi wanajiuliza itakuwa Real madrid ya aina gani,huku Christiano Ronaldo huku Bale.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.