Baada ya Cristiano Ronaldo kusaini mkataba wa nyongeza na Real Madrid,mkataba huo una maana kuwa sasa mchezaji huyo ni zaidi ya nyota wa Barcelonas Lionel Messi.
Ronaldo mshahara wake ni Euro milioni 17 kwa mwaka kwa miaka mitano ijayo wakati Messi mshahara wake ni Euro milioni 13 kwa mwaka.
Ronaldo, ambaye mkataba wake wa awali ulibaki miaka miwili ilielezwa kuwa alitaka kuondoka Madrid kwenye usajili uliopita wa majira ya joto akihusishwa na Manchester United na Paris Saint-Germain.
Lakini Ronaldo mwenyewe alipokuwa akizungumza wakati wa kutangazwa kuongezewa mkataba akasema ana furaha ya kuendelea kuwepo kwenye klabu hiyo na ataendelea kuwepo kwa miaka mingine mitano zaidi na anataka kushinda mataji na anataka kuonesha uwezo wake uwanjani.
Akiizungumzia Manchester United akasema kila mtu anajua alikuwa kwenye klabu hiyo kwa miaka sita lakini klabu hiyo zama zake zimepita na sasa klabu yake ni Real Madrid,hapo ndio nyumbani kwake hata familia yake iko hapo.
Anasema anazisheshimu klabu zote zilizokuwa zinamuhitaji lakini maamuzi yake yanafahamika kwamna ni kuitumikia Real Madrid ikiwezekana mpaka mwisho wa maisha yake ya soka.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.