Tuesday, September 10, 2013

Lampard mechi 100

Boss wa England Roy Hodgson amethibitisha kuwa kiungo Frank Lampard atatimiza mechi yake ya 100 kuichezea timu ya Taifa atakapomchezesha kwenye mchezo dhidi ya Ukraine leo.

Kiungo huyo wa Chelsea mwenye miaka 35,atakuwa mchezaji wa nane wa England Three Lions kufikisha mechi hizo akiungana na Steven Gerrard na Ashley Cole.
Hodgson amesema kwenye mchezo wa leo atafanya mabadiliko ya nafasi moja kutoka kwenye kikosi kilichoichapa Moldova mabao 4-0,ambapo kiungo James Milner atambadili Danny Welbeck.
England wanaongoza kundi H lakini wanaweza kuzidiwa kama watafungwa na Ukraine.

Waliofikisha mechi 100 England

125: Peter Shilton (1970-1990)
115: David Beckham (1996-2009)
108: Bobby Moore (1962-1973)
106: Bobby Charlton (1958-1970)
105: Billy Wright (1946-1959)
104: Ashley Cole (2001-present)
104: Steven Gerrard (2000-present)

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.