Wednesday, September 4, 2013
Ozil aitajirisha klabu ya daraja la nne
Timu ya daraja la nne ya Rot-Weiss Essen ya nchini Ujerumani itahusika kuutafuna mpunga wa uhamisho wa Mesut Ozil aliyeweka rekodi ya usajili kwenye klabu ya Arsenal akitokea Real Madrid.
Ozil alianza maisha yake ya soka kwenye klabu hiyo iliyowahi kushiriki ligi kuu ya Ujerumani Bundesliga kabla ya kuelekea Schalke 04 yenye maskani yake kwenye mji wa Gelsenkirchen akiwa na miaka 16 mwaka 2005 na mwaka mmoja baadaye August 12, 2006,akaanza kucheza ligi kuu ya Ujerumani kwenye mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Frankfurt.
Baada ya kucheza michezo 30 akiwa na Schalke, Ozil akatimkia zake Werder Bremen mwaka 2008,na baadaye akaenda zake Real MaDRID.
Kwa mujibu wa tarataibu za FIFA Rot Weiss Essen itafaidika na asilimia 5 inayotolewa kama fidia ya kumuandaa mchezaji huyo ambayo pia itatafunwa na Schalke ,Werder Bremen na Real Madrid.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.