Mabondia Francis Cheka na Francis Miyeyusho leo wametinga kwenye bunge la jamhuri ya Muungano wa Tanzania mjini Dodoma.
Cheka ametinga na mkanda wake wa ubingwa wa WBU aliomchapa bondia kutoka nchini Marekani Phil Williams wakati Miyeyusho ametinga na mkanda wake wa ubingwa wa WBF uzito wa bantam.
Naibu Spika Job Ndugai akizungumza baada ya kuwatambulisha amewapa hongera kwa kuendelea kupeperusha vyema bendera ya Tanzania na akiwataka kuendelea na mwendo huo wa mafanikio.
Ndugai amesema mabondia hao ni mfano wa kuigwa na mabondia wengine pamoja na wanamichezo kiujumla.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.