Friday, September 6, 2013
LUIZ : Nimechagua Chelsea,Barcelona hapana
Beki kisiki raia wa Brazil DAVID LUIZ amefichua kuwa aliamua kuipiga chini ofa ya kuondoka Chelsea kwenda Barcelona tena iliyopelekwa kiofisi.
Luiz, 26, anasema wachezajai wenzake wanaocheza timu hiyo Neymar na Daniel Alves walikuwa wakimshawishi kufanya hivyo lakini binafsi hakutaka kwenda kwenye timu hiyo.
Barcelona walihusishwa kumtaka beki huyo ili kuziba pengo la beki wake mkongwe Carlos Puyol,ambaye ni majeruhi lakini Luiz ambaye kwasasa yupo kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Brazil anasema aliamua kubakia Stamford Bridge.
Ili kumchukua beki huyo Barcelona walikuwa tayari kutoa kitita kinene cha paundi milioni 65 ambacho kingekuwa ni kitita cha rekodi kwa beki kununuliwa kwa bei ya juu.
Luiz anasema anajisikia furaha kuwepo kwenye timu kubwa akiwa na imani kuwa watachukua ubingwa wa Ulaya,akiona ni jambo zuri kuvikwepa vigogo kwenye hatua ya makundi.
Anasema ni mashindano magumu yanayokutanisha timu kali lakini ni vizuri hatua ya makundi usikutane na vigogo wenzako.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.