Wednesday, September 11, 2013

Ferrari rasmi kwa Raikkonen,Massa akitangaza kutoka

Kimi Raikkonen ataungana rasmi na Fernando Alonso kutengeneza timu ya Ferrari mwaka 2014 huku Felipe Massa akitangaza kuondoka.

Raikkonen aliyewahi kushinda taji la dunia akiwa na Ferrari mwaka 2007 aliondoka kwenye timu hiyo nafasi yake ikichukuliwa na Alonso mwaka 2009,amesaini mkataba wa nmwaka mmoja utakaodumu mpaka 2015.
Baada ya Raikkonen, 33,kujiunga kwenye timu hiyo,Massa kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter ametangaza kuondoka kwenye timu hiyo mwishoni mwa msimu wa Formula1.

Massa raia wa Brazil amesema kuanzia 2014 hatakuwa dereva wa timu ya Ferrari aliyoanza kuitumikia tokea mwaka 2006.


Maamuzi ya kutengeneza timu moja ya Alonso na Raikkonen kunabadilisha falsafa ya Ferrari,ambao huko nyuma walikuwa wanatumia dereva mmoja mwenye nguvu kuanzia enzi za Michael Schumacher 1996-2006 na Alonso kwa miaka minne iliyopita.

Ferrari sasa imeamua kuwa na madereva wawili wote wakali wakiona ni njia nzuri zaidi ya kuzitesa timu nyingine kama ilivyokuwa sera yao wakati wa Raikkonen na Massa 2007-9.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.