Sunday, September 22, 2013

EPL : Man City waifumua Man United ya Moyes,Arsenal wajitanua kileleni

Manchester United leo wameonja joto ya jiwe baada ya kula kisago kizito cha mabao 4-1 kutoka kwa mahasimu wao Manchester City kwenye mchezo wa ligi kuu ya EPL uliopigwa Etihad Stadium.

Mabao ya City yametumbukizwa wavuni na Sergio Arguelo aliyetupia mawili,Yaya Toure na Samir Nasri huku lile la United likiwekwa wavuni na Wayne Rooney.
Katika michezo mingine Arsenal wamerejea kileleni baada ya kuwachapa Stoke City kwa mabao 3-1,huku Tottenham wakikalia nafasi ya pili baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cardif bao likifungwa na Paulinho.

Arsenal na Spurs wote wana pointi 12 huku City,Chelsea,Liverpool wakifuatia wakiwa na pointi 10 kila mmoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.