Shirikisho la soka nchini TFF limesema limepokea barua ya rufaa kutoka kwa mabingwa watetezi wa ligi kuu soka Tanzania bara Yanga Africa,lakini shirikisho hilo halihusiki na vurugu hizo.
Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema TFF haihusiki na vurugu zozote zinazotokea nje ya uwanja kwakuwa haziwahusu zinalihusu jeshi la Polisi.
Wambura amesema kama kuna vurugu zilitokea nje na vioo vya magari kuvunjwa hilo ni suala la jeshi la Polisi na ndicho Yanga walichotakiwa kukifanya na si kukimbilia kwa TFF.
Amesema kwa mujibu wa kanuni na utaratibu wa mpira vurugu zozote zinazotokea ndani ya uwanja ndizo wanazohusika nazo na kuzitolea maamuzi,kwahiyo wataipeleka rufaa hiyo ya Yanga kwenye kamati inayohusika na kutazama lile linalowahusu ili kulitoea maamuzi.
Katika rufaa hiyo Yanga wameomba mchezo wao dhidi ya Mbeya City urudiwe katika uwanja huru kwakuwa walifanyiwa vurugu kabla ya mchezo hali iliyowaharibu kisaikolojia na kupeleka kutoka sare ya kufungana bao 1-1.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.