Wednesday, September 18, 2013

LIGI KUU : Simba kileleni,Tambwe apiga hat trick,Yanga yakamatwa,Ashanti nao waanza

Ligi kuu soka Tanzanaia bara imeshuhudia Wekundu wa msimbazi Simba wakikwea kileleni baada ya kuondoka na ushindi mzito wa mabao 6-0 dhidi ya Mgambo JKT kwenye uwanja wa Taifa huku mshambuliaji wake mpya Hamis Tambwe akianza kazi ya kupachika mabao akitupia hat trick baada ya kutupia wavuni mabao manne.

Mabao mengine ya Simba yaliwekwa wavuni na kinda haroun Chanongo.

Ushindi huo unawapandisha Simba kileleni mwa ligi hiyo baada ya maafande wa JKT Ruvu kukubali kipigo cha bao 1-0 mbele ya Ruvu shooting kwenye mchezo uliopigwa uwanja wa Mabatini Mlandizi.

Mabingwa watetezi Yanga Africa wamerudia kile walichokipata kwenye mchezo uliopita baada ya kualizmishwa sare na maafande wa Tanzania Prisons kwenye uwanja wa Sokoine.

Huko Mkwakwani Tanga Coastal Unuion wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Rhino Rangares wakati huko Manungu Mtibwa Sugar nao wamekomaliwa na Mbeya City wakilazimishwa suluhu ya bila kufungana.

Huko Kaitaba Kagera Sugar wameutumia vyema uwanja wake wa nyumbani wakiibuka na ushindi wa mabao 2-1 wakati Ashanti United wamefanikiwa kuvuna pointi yao ya kwanza kwenye ligi kuu wakipata sare ya kufungana bao 1-1 sterring akiwa Anthon Matangalu aliyekwamisha bao hilo dakika ya 79 baada ya Azam kutangulia kwa bao la Kipre Tchetche.

Nahodha wa Azam Aggrey Morris alioneshwa kadi nyekundu.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.