Monday, September 23, 2013

Sunderland yamtimua kazi Di Canio

Kocha Paolo Di Canio ametimuliwa kazi ya kuifundisha Sunderland baada ya mechi 5 tokea kuanza kwa ligi.

Taarifa ya Sunderland inasema kibarua cha kuifundisha timu hiyo amepewa kocha wa muda Kevin Ball atakayeanza kukiongoza kikosi hicho kuanzia mchezo wa leo wa michuano ya Capital One dhidi ya Peterborough United na baadaye atatajwa kocha wa kurithi mikoba ya Di Canio.

 Klabu hiyo imemshukuru Di Canio na jopo lake na kuwatakia kila lakheri mbele waendako.

Kocha huyo ameshinda mechi 2 kati ya mechi 12 za ligi kuu ambazo Sunderland imecheza ikiwa chini yake tokea amejiunga msimu uliopita.

Roberto Mancini na Roberto Di Mateo wanatajwa kupewa mikoba ya kukinoa kikosi hicho ambacho kinaburuza mkia kikiwa na pointi 1 baada ya michezo mitano.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.