Tuesday, September 10, 2013

UBADHIRIFU : Lipuli yawashtaki Simba


Na Fatma Abdallah Chikawe

Uongozi wa timu ya Lipuli ya Iringa umewashtaki kwa shirikisho la kabumbu nchini TFF Wekundu wa Msimbazi Simba wakipinga ubadhirifu wa fedha unaodaiwa kufanywa na baadhi ya watendaji wa Wekundu hao kwenye mchezo wao wa kirafiki uliopigwa mwishoni mwa wiki iliyopita kwenye uwanja wa Kinesi huku Simba wakiibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Lipuli inayonolewa na nahodha wa zamani wa Yanga na Timu ya taifa ya Tanzania Taifa stars Shadrack Nsajigwa iliutumia mchezo huo kujiandaa na ligi daraja la kwanza itakayoanza September 14 mwaka huu wakati Wekundu wa msimbazi Simba waliutumia mchezo huo kama sehemu ya maandalizi yake ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Wakata miwa wa Mtibwa Sugar utakaochezwa uwanja wa Taifa Jumamosi.
Mwenyekiti wa Lipuli Abuu Changawa amesema kitendo walichofanyiwa na Simba hakikuwa cha kiungwana hata kidogo na hawako tayari kuendelea kukaa kimya.

Changawa amesema kutokana na kitendo hicho hawatakuwa tayari kucheza mchezo mwingine wowote na Simba.
Kwa upande wa Simba Kaimu makamu mwenyekiti wake Joseph Itang’are Kinesi amesema hausiki na lolote katika hilo na kama kuna lolote ambalo Lipuli hawakuridhika nalo ni vyema wangekaa kuzungumza kuliko kulalamika.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.