Friday, September 6, 2013
TENNIS : Murray nje,Djokovic ndani
Bingwa mtetezi wa mashindano ya US Open Andy Murray ndoto zake za kutetea taji hilo zimeyeyuka baada ya kupoteza mchezo mbele ya MSwiss anayekamata nafasi ya tisa kwenye ubora wa viwango Stanislas Wawrinka katika mchezo wa robo fainali.
Murray ameshindwa kupata ushindi katika seti hata moja baada ya kupoteza kwa 6-4 6-3 6-2 huko Arthur Ashe Stadium.
Wawrinka mwenye miaka 28 ametinga hatua ya nusu fainali ambayo atacheza na kinara wa dunia kwa wanaume Novak Djokovic ambaye amemshinda MRussia anayekamata nafasi ya 21 Mikhail Youzhny kwenye mchezo mwingine wa robo fainali.
Djokovic, 26,ameshinda kwa 6-3 6-2 3-6 6-0 na kutinga hatua ya nusu fainali kwa mara ya saba mfululizo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.