Wednesday, September 18, 2013

Del Piero ala pensheni ya uzeeni


MTALIANO Alessandro Del Piero ametajwa rasmi kama nahodha wa timu ya Sydney FC ya Australia.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa kibibi kizee cha Torino Juventus ama Juve ndiye mchezaji aliyesajiliwa kwa usajili mkubwa zaidi nchini Australia na akisababisha kuongezeka kwa mashabiki uwanjani,watazamaji wa Tv na ufuatiliaji wa vyombo vya habari.

Ikiwa kama zawadi ataiongoza timu hiyo Sydney msimu wa 2013/14 unaotaraji kuanza kuunguruma October,baada ya kumbadili nahodha wa awali Terry McFlynn.

Del Piero mwenye miaka 38 ametumia miaka 19 akiwa na Juventus na alijiunga na Sydney mwaka uliopita akiifungia mabao 14.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.