Friday, September 13, 2013
Qatar wakomaa na kombe la dunia 2022
Katibu mkuu wa kamati ya fainali za dunia za mwaka 2022 zitakazofanyika Qatar Hassan Al-Thawadi amepinga fainali hizo kupelekwa kwenye nchi nyingine.
Shirikisho la soka la dunia FIFA linaweza kusogeza mbele fainali hizo za dunia mpaka kipindi cha majira ya baridi kuepukana na hali ya joto nchini humo.
Mwenyekiti wa FA Greg Dyke amesema kama haitawezekana kuisogeza wakati wa baridi inafaa kuhamishia nchi nyingine jambo ambalo linapingwa na Al-Thawadi anayesema haoni kwanini Qatar isiandae fainali hizo za mwaka 2022.
Rais wa Fifa Sepp Blatter anafikiria fainali hizo zisogezwe mpaka wakati wa majira nya baridi kutokana na joto la Qatar kufikia mpaka 50C wakati wa majira ya joto.
Blatter, 77,amekiri kuwa yawezekana FIFA ilikosea kuipa nchi hiyo uwenyeji wa fainali hizo za mwaka 2022.
Lakini Al-Thawadi anasisitiza kuwa Qatar ni sehemu sahihi akisema wanawakilisha mashariki ya kati kwahiyo inafaa kuendelea kuwepo katika nchi hiyo kwakuwa mashariki ya kati wanastahili kuwa wenyeji wa frainali hizo kubwa za dunia.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.