Chelsea na Tottenham Hotspur wanaingia katika majaribu ya kuwania taji la ubingwa wa ligi ya England EPL wakati watakapokutana uso kwa uso kesho huko White Hart Lane.
Timu zote mbili zimefanya usajili wa kuongeza nguvu kwenye vikosi vyao lakini wananza kampeni ya kulisaka taji hilo huku wakikumbuka kukutana mara 149.
Bao lililotumbukizwa wavuni dakika za majeruhi na Paulinho liliipa Spurs ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Cardiff City
wikiendi iliyopita na kuifanya ifikishe pointi 12 sawa na Arsenal wakati Chelsea walipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Fulham na kuwafanya kufikisha pointi 12 ikiwa ni pointi 2 nyuma ya Arsenal na Spurs.
Lakini mchezo huo pia utawakutanisha tena kwa mara nyingine makocha Andre
Villas-Boas na Jose Mourinho wanakutana kwa mara ya kwanza katika ligi kuu ya England.
AVB anakutana na timu yake ya zamani ambayo aliwahi kuitumikia kabla ya kuoneshwa mlango wa kutokea na sasa anakutana nayo ikiwa na kocha tofauti lakini anayemfahamu vizuri.
Hata hivyo beki wa kati wa Chelsea David Luiz,ambaye amecheza mechi moja tu ya ligi chini ya Mourinho anasema si sahihi kuigusa mechi hiyo na kusema ni Mourinho dhidi ya Villas Boas hiyo mechi ni Chelsea dhidi ya Tottenham.
Anasema itakuwa mechi kali inayokutanisha mahasimu,ni mchezo ambao kila mmoja atautazama na kila mmoja anataka kucheza mchezo huo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.