Akitangaza maamuzi ya kikao cha kamati ya utendaji ya Yanga iliyokutana jana Makamu mwenyekiti wa yanga Clement Sanga amesema Naggi anaingia kwenye sekretarieti ya klabu hiyo ikiwa ni njia za kuboresha utendaji wa klabu.
Sanga amesema mbali ya Naggi kuna viongozi wengine waliowaongeza kwenye sekretarieti akiwemo Benno Njovu anayeingia kama mshauri wa uongozi na fedha na George Magani.
Akizungumzia kuhusiana na Naggi aliyetiliwa shaka juu ya uwanachama wake kwa klabu hiyo amesema taratibu zinafanyika ili kumpatia uwanachama wa klabu hiyo japo kwa sasa ni shabiki mkubwa wa Yanga.
Hata hivyo Sanga amepiga chenga kuhusiana na nafasi sahihi ya Naggi kwenye klabu hiyo akisema kiongozi huyo anaingia kwenye sekretarieti wakati wanatazama sehemu watakayomuweka baada ya kupata uwanachama huku akiongeza kuwa katibu mkuu aliyemaliza muda wake Lawrance Mwalusako naye bado yupo.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.