Beki wake mpya Martin Demichelis aliyesajiliwa kutokana na mabeki wa kati kukumbwa na masahibu ya majeruhi naye ameumia goti na atakaa nje kwa wiki sita.
Beki huyo raia wa Argentina aliyesajiliwa kutokea Atletico Madrid kuumia kwake kumemshtua kocha wa City Manuel Pellegrini,aliyegundua kuwa hataweza kumtumia beki huyo mpaka mwezi November.
Demichelis ameumia mazoezini na vipimo vinaonesha kuwa hatalazimika kufanyiwa upasuaji.
Pellegrini anakabiliwa na uhaba wa mabeki wa kati baada ya nahodha wake Vincent Kompany akiwa bado majeruhi,Micah Richards bado hajawa sawa.
Ukiwaondoa Joleon Lescott na Matija Nastasic,sasa Pellegrini anaweza kuwatumia beki wa Hispania Javi Garcia, au kinda raia wa Ubelgiji Dedryck Boyata,
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.