Serena mwenye miaka 31,amepata ushindi wenye upinzani wa 7-5 6-7 (6-8) 6-1 akirejea ushindi wake wa mwaka uliopita dhidi ya Azarenka.
Mwanadada huyo sasa anahesabu taji lake la 17 la Grand Slam kwa mchezaji mmoja mmoja akiwa nyuma ya Martina Navratilova na Chris Evert,wenye mataji 18 na saba nyuma ya Margaret Court anayeongoza akiwa na mataji 24.
Kwa upande wa wanaume Rafael Nadal na mchezaji namba moja wa dunia Novak Djokovic wanakutana katika fainali leo Jumatatu.
Wanakutana kwa mara ya 37 ,mara sita ikiwa katika fainali za Grand Slam.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.