Tuesday, September 3, 2013

Rekodi mpya ya usajili Ulaya yaandikwa


Klabu za ligi kuu ya England zimetumia kiasi cha paundi milioni 630 katika usajili uliofungwa jana na kuweka rekodi mpya.

Rekodi ya awali ilikuwa ni paundi milioni 500 iliyowekwa mwaka 2008.

Miongoni mwa usajili mkubwa uliotikisa ni pamoja na ule wa Mesut Ozil kutoka Real Madrid kwenda Arsenal kwa ada ya paundi milioni 42.4.
Manchester United nao wakajitutumua dakika za lala salama wakimnasa kiungo wa kutokea Everton Marouane Fellaini kwa ada ya paundi milioni 27.5.
 
Usajili wa sasa ni usajili ulioweka rekodi ya klabu kutumia zaidi lakini pia ni msimu ulioweka rekodi ya dunia kwa mchezaji kununuliwa kwa bei ghali.
Rekodi hiyo ni ya Gareth Bale aliyetua Real Madrid kwa dau la paundi milioni 85 akitokea Spurs.
La Liga na Serie A wametumia paundi milioni 335, Ufaransa Ligue 1 paundi milioni 315 na Ujerumani Bundesliga paundi milioni 230.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.