Monday, September 9, 2013

ITALIAN GRAND PRIX : HAMILTON asema ilikuwa weekend ngumu kwake

Dereva wa magari wa Mercedes kwenye Formula1 Lewis Hamilton amesema hajasalimu amri wala kukata tamaa kusaka taji la ubingwa wa dunia licha ya kumaliza nafasi ya 9 kwenye Italian Grand Prix.
Kwenye mashindano hayo dereva wa Red Bull Sebastian Vettel alipata ushindi uliompa taji lake la 6 na ikiwa ni pointi 81 zaidi ya Hamilton.

Hamilton anasema alipotoka kwenye gari alikuwa na hasira lakini akapata nguvu na kusema hajakata tamaa.
Dereva huyo maarufu alianzia nafasi ya 12 baada ya kufanya vibaya kwenye majaribio ambayo hakuingia hata kwenye kumi bora na nasema hilo lilimfanya aendeshe gari kama mpumbavu na anakiri ilikuwa wikiendi ngumu kwake.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.