Monday, September 16, 2013

MAYWEATHER,timu ya hela,timu isiyopoteza,nyota kibao,wa show lov,Bieber,Lil Wayne nao ndani

Nyota kibao wanaonekana wanamkubali sana Bingwa wa WBC na WBA Floyd Mayweather ambaye rekodi yake imeendelea kusimama akicheza michezo 45 bila kupoteza pambano,katika mchezo ambao amefichua siri kuwa bila ya kuwepo familia yake angechezea kichapo mbele ya bondia Saul Alvarez.
Mayweather mwenye miaka 36,anasema wakati akiendelea kupigana kiwiko kiliteguka lakini kila alipokuwa akiitazama familia yake ilikuwa inampa nguvu za kuendelea kupigana na kuvumilia hali tete aliyokuwa nayo.
Alisindikizwa na msanii wa muziki Justin Bieber
Nyota mbalimbali wakiwemo nyota wa muziki duniani wanaonekana ni mashabiki wakubwa wa bondia huyo baada ya kuonekana wakipongeza na kuunadi ushindi wake kwenye mtandao wa kijamii wa twitte,lakini hata wakati akiingia ulingoni Mayweather alisindikizwa na Justin Bieber na Lil Wayne.

Nyota wengine walio show lov kwa Mayweather kwenye mtandao wa kijamii wa twitter ni pamoja na Eva Longoria, Kat Dennings,John Cusack,Michelle Rodriguez na Joe Rogan.

Bieber akiwa amepozi kwa picha baada ya pambano




 
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.