Nahodha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Jella Mtagwa amepewa cheti cha umiliki wa ardhi na nyumba kutoka kwa mtandao wa wasanii Tanzania SHIWATA.
Mtagwa amekabidhiwa eneo la robo ekari ambalo anatarajia kujenga nyumba kubwa.
Mkuu wa wilaya mstaafu,Henry Clemence ndiye aliyekuwa mgeni rasmi katika sherehe ya kukabidhi nyumba hizo 38 za wasanii wa Mtandao wa Wasanii Tanzania SHIWATA zilizopo katika kijiji cha Mwanzega, Mkuranga.
Itakumbukwa Mtagwa amekuwa na kilio cha kumsomesha mtoto wake huku yeye binafsi akiwa hana makazi yake binafsi ya kuishi,kilio ambacho kilisikika na kufanyiwa kazi.
Nahodha huyo wa zamani wa Stars ndiye mchezaji mwenye historia ya sura yake kutumika kwenye stamp za kutumia barua za shirika la Posta nchini.
Katika timu ya Taifa Mtagwa amewahi kucheza na Rais wa Shirikisho la soka nchini TFF anayemaliza muda wake Leodger Tenga.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.