Friday, September 20, 2013

Baada ya kupiga Hat trick TFF yampotezea Tambwe,yasema hakuna kanuni ya kumpa mpira


Shirikisho la soka nchini TFF limemtetea mwamuzi wa mchezo wa Simba na Mgambo JKT kwa kutompatia mpira mshambuliaji wa Simba Amis Tambwe aliyetupia wavuni mabao manne.

Afisa habari wa TFF Boniface Wambura amesema hakuna sheria yoyote ya FIFA inayosema mchezaji akifunga mabao matatu atapewa mpira.

Amesema mchezaji anayepewa mpira baada ya kutupia bao tatu huwa inatumika mchezo wa kiungwana "Fair Play" katika kumpa mpira huo lakini hakuna kanuni inayolazimisha kufanya hivyo.

Hata hivyo Wambura amesema watapanga siku ambayo watampatia mpira Taambwe kama sehemu ya mchezo wa kiungwana na si kwa kulazimishwa na kanuni.

Tambwe alipiga bao nne kwenye mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mgambo JKT uliopigwa Jumatano kwenye uwanja wa Taifa na baada ya mchezo alimpomfuata mwamuzi ampatie mpira hakuweza kupewa mpaka maagizo yatoke kwa TFF jambo ambalo lilizua mjadala.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.