Thursday, September 5, 2013
Ashanti yaanza kukoga fedha,yalamba udhamini mwingine wa Azam
Timu ya Ashanti United imelamba udhamini kutoka kwa kampuni ya Azam kupitia kinywaji chake cha Malta.
Mkataba huo wa Azam kupitia kinywaji cha malta na Ashanti una thamani ya shilingi milioni 35 kwa mwaka.
Afisa habari wa Ashanti Rajab Marijan amesema udhamini huo ni muhimu kwao kwakuwa unasaidia kupunguza baadhi ya gharama za kuiendesha timu hiyo.
Udhamini huo unaongeza mapato kwa Ashanti ambao tayari wana uhakika wa shilingi milioni 100 kwa mwaka kutoka kwa Azam Tv na pia fedha za kutoka kwa mdhyamini wa ligi kuu kampuni ya simu za mikononi ya VodaCom.
Ashanti imerejea ligi kuu msimu huu ikiwa pamoja na Mbeya City ya Mbeya na Rhino Rangers ya Tabora,japo imecheza mechi mbili za ligi dhidi ya Yanga na JKT Mgambo na zote imepoteza.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.