Monday, September 16, 2013

Sturridge aipa kiburi Liverpool,Suarez majanga,Rodgers asema anayejiona star mlango uko wazi

Kocha Brendan Rodgers amemuonya Luis Suarez akimwambia atakaporejea kikosini hatakuwa mshambuliaji wa kwanza kirahisi kwenye kikosi hicho.

Suarez anatumikia adhabu ya kufungiwa mechi 10 baada ya tukio la kumngáta beki wa Chelsea Branislav Ivanovic,na sasa kwenye kikosi cha Liverpool Daniel Sturridge anaonekana ndio mshambuliaji namba moja akiifungia timu hiyo kwenye mechi zote tatu walizocheza.

Nafasi hiyo ya kupachika mabao kwenye msimu uliopita ilibeba na Suarez lakini Rodgers anasema hakuna nyota kikosi chake cha Liverpool,anasema si Suarez wala Sturridge atakayekuwa muhimili wa timu,kila mmoja anapewa jukumu la kutekeleza uwanjani.

Rodgers anasema yeyote anayejiona superstar,anaweza kuondoka kwakuwa kwasasa wanatengeneza timu na si mtu mmoja mmoja.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.