Wednesday, September 11, 2013

Barcelona yagonga hodi Chelsea

Barcelona wanafikiria kugonga hodi Chelsea ili kumnasa golikipa wake namba moja Petr Cech wanayetaka awe mbadala wa Victor Valdes.
 
Cech amefanya mazungumzo na kocha wa Chelsea Jose Mourinho ambaye bado anaamini kipa huyo ni mmoja wa makipa bora duniani katika wakati ambao Thibaut Courtois, 21,ambaye yupo kwenye mwaka wake wa tatu kwa mkopo huko Atletico Madrid akichukuliwa kama mbadala wake.
Ripoti kutoka Hispania zinasema kuwa Chelsea na Barcelona wanawea kukubaliana uhamisho utakaowahusu Cech na Valdes kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January.
Lakini Mourinho hana mpabngo wa kumruhusu Cech kuondoka katikati ya kampeni yake wakati pia mchezaji mwenyewe anatamani kubaki kwenye kikosi hicho mpaka mwisho wa msimu.
Barcelona pia wanataka kumsajili golikipa Pepe Reina wa Liverpool anayecheza kwa mkopo Napoli ya Italia na inaelezwa kuwa tayari kipa huyo amesaini mkataba wa awali na Barcelona lakini taarifa ya kwamba wanaweza kumpata Cech inawafanya kupitia upya uamuzi wao.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.