Thursday, September 12, 2013

Barcelona wapiga hesabu kwa Mata

BARCELONA wanataka kujaribu kumnasa kiungo Juan Mata kutokea Chelsea wakiendelea kufuatilia kwa karibu nyendo zake mpaka wakati wa dirisha dogo mwezi January,lakini wanaweza kukumbana na ugumu kutoka kwa kocha Jose Mourinho.
Ripoti kutoka nchini Hispania zinasema Barca wamemtathimini Mata na kuona ni mchezaji anayeweza kuendana na style yao na inaonekana pia ni mbadala wa Alexis Sanchez au Cesc Fabregas.
 
Mata amehusishwa pia kutakiwa na Arsenal na Tottenham wakati wa usajili wa majira ya joto lakini mchezaji na klabu yake walipingana na taarifa hizo.

Licha ya Mata mwenyewe kukiri ana furaha Chelsea lakini inaelezwa kuwa Mourinho bado haridhiki na mwenendo wa kiungo huyo mwenye miaka 25 na anaendelea kumfuatilia kama hatabadilika kufikia January anaweza kufikiria kumuuza.

Mata,mwenyewe kwasasa anatupia jicho lake kwenye fainali za kombe la dunia mwakani nchini Brazil na anaweza kufikiria kuondoka kama ataona anaendelea kusugua benchi darajani kunakohatarisha nafasi yake ya kuitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Hispania.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.