Monday, September 2, 2013

Baada ya Bale sasa Madrid walichokonoa kwa Suarez


Leo ikiwa siku ya mwisho kwa usajili wa wachezaji barani Ulaya,Real Madrid baada ya kuhitimisha usajili wao ulioweka rekodi wa kumsajili Gareth Bale kwa paundi milioni 86 sasa wanataka kumchukua mshambuliaji wa Liverpool Luis Suarez kwa dau la paundi milioni 45.

Real wako tayari kutoa fedha pamoja na mchezaji ili kukamilisha mpango wao wa kumnasa mshambuliaji huyo raia wa Uruguay ambaye kwenye mkataba wake kuna kipengele kinachomruhusu kuondoka kama timu itafikia kiwango cha paundi milioni 40.
Suarez alijaribu kulazimisha kuondoka kwenye klabu hiyo kwenda ARSENAL lakini ikashindikana na sasa suala lake likimalziwa na ikionekana mwenye furaha kwenye klabu hiyo ya huko Merseyside.
Suarez amefunga mabao 33 kwa klabu hiyo na timu ya taifa msimu uliopita ikimfanya kuwa mmoja wa washambuliaji hatari duniani na kwenye klabu ya Liverpool jambo linalowafanya Liverpool kuwa kwenye presha kubwa ya kuendelea kukaa kwenye klabu hiyo ambayo tayari imesema hauzwi.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.