Monday, September 9, 2013

MAANDALIZI YA KUMKOSA ROONEY : Moyes aanza kumpigia hesabu Benteke

David Moyes anafahamu kuwa siku za usoni atamkosa mshambuliaji Wayne Rooney na Christian Benteke ndiye anampigia hesabu za kumchomoa Aston Villa ili awe mbadala wake.
Moyes ni mshabiki mkubwa wa mshambuliaji huyo wa kati mwenye nguvu na anayefanya vizuri kwenye ligi kuu ya England.
 
Kocha huyo anafahamu fika kuwa timu yake inakabiliwa na tatizo la mshambuliaji mrefu na imara na anafikiria kuwa anaweza kumpoteza Rooney mmoja wa washambuliaji wenye msuli wa kutosha.
Moyes alikuwa akiitazama shughuli ya Benteke, 22,wakati akiichezea timu yake ya Taifa dhidi ya Scotland Ijumaa iliyopita. 
Villa wamemuongezea mkataba mshambuliaji huyo mwezi July na sasa analipwa paundi elfu 60 kwa wiki baada ya kuomba kuondoka.
 
United wanatazama kumnasa mshambuliaji huyo wakati wa dirisha dogo mwezi January.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.