Gareth Bale yupo karibu kusaini mkataba mwingine wa mamilioni ikiwa ni wiki zipatazo tatu baada ya kuwa mchezaji ghali zaidi duniani.
Adidas,ambao wamekuwa na Bale tokea akiwa na miaka 16,wanaamini atakubali kuongeza mkataba wa muda mrefu ili kuendelea kuvaa viatu vyenye nembo ya kampuni hiyo.
Mkataba wa Bale na kampuni hiyo upo katika mwaka wa mwisho kumalizika na thamani yake inaonekiana kuongezeka zaidi kwakuwa yupo kwenye timu ambayo inacheza Champions legue.
Kusaini mkataba mrefu inaendeleza vita ya mafanikio kwa Bale na Christiano Ronaldo ambaye kwasasa anatisha na matangazo akionekana kwenye mabango ya kampuni pinzani ya NIKE.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.