Friday, September 13, 2013

Adebayor atupwa kujifua kwa wachezaji wa benchi

Mshambuliaji Emmanuel Adebayor ametakiwa kufanya mazoezi na wachezaji wanaolisugua benchi wa Tottenham.
 
Roberto Soldado ndiye amekuwa mshambuliaji chaguo la kwanza la Spurs akitua kwenye timu hiyo kwa dau lililoweka rekodi ya klabu hiyo la paundi milioni 26 akitokea Valencia huku Jermain Defoe akiwa anamsaidia mshambuliaji huyo namba moja.
 
Adebayor hajacheza mchezo wa ushindani ukiondoa kwenye mechi za kujiandaa na msimu na likizo yake ya kufiwa na kaka yake huko Togo iliongezwa.
Mshambuliaji huyo alirejea London mwezi uliopita lakini akarejea tena barani Africa kwa kile ambacho kocha André Villas-Boas akielezea ni matatizo binafsi.
 
Adebayor mwenye miaka 29 anatarajia kujiunga tena na Spurs Jumatatu na atajiunga kwenye mazoezi ya wachezaji wanaolisugua benchi.
 
Mshambuliaji huyo ambaye alisaini mkataba wa kudumu katika timu hiyo baada ya kucheza kwa mkopo inaonekana si mshambuliaji chaguo la kwanza kwa AVB kwasasa.
 
AVB ambaye amemuuza Gareth Bale kwenda Real Madrid kwa dau la paundi milioni 85.3 amesaini wachezaji saba kwenye usajili wa majira ya joto.
 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.