Monday, September 23, 2013

Lukaku afungiwa milango Chelsea

Wakati mshambuliaji Lomeu Lukaku akiota kurudi kuichezea Chelsea iliyompeleka kwa mkopo Everton,kocha wa the blues Jose Mourinho amepigilia msumari mzito akithibitisha kuwa hakuna uwezekano wa mshambuliaji huyo kurudi darajani msimu huu.

Mourinho anasema mshambuliaji huyo ataendelea kubaki huko Goodison Park mpaka mwisho wa msimu mwezi May.
 
Lakini kocha huyo akasema Lukaku ni mzuri  Everton na kama ataendelea kucheza kila mchezo itamjengea mazingira mazuri ya baadaye kwa Chelsea.

Wikiendi Lukaku aliisaidia Everton kuichapa West Ham baada ya kutupia bao la ushindi katika mchezo ambao ulikuwa na misukosuko kwake baada ya kuumia wakati anafunga na akisema hata hakufahamu kama ni yeye ndiye kafunga hilo goli.
 
 

Chelsea kwasasa katika safu ya ushambuliaji wana Samuel Etoo,Fernando Torres na Demba Ba wanaogombea namba. 

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.