Friday, September 20, 2013

Mashabiki Ajax marufuku kwenda kwa PSV


Mashabiki wa timu ya Ajax wamekosa haki yao ya kimahakama ya kutaka kupindua kuzuiwa kwa mashabiki wake kuhudhuria mchezo wa ligi kuu ya Uholanzi dhidi ya mahasimu wao PSV Eindhoven.

Ajax ilitaka mashabiki wake waruhusiwe kwenda Eindhoven kwa basi baada ya safari ya treni maalumu kutoka Amsterdam kufutwa.

Meya wa Eindhoven Rob van Gijzel alikataa mpango huo baada ya kuhofia vurugu za mashabiki.

Ajax wanasema waliona umuhimu kwa mashabiki wao kuhudhuria katika kila mchezo ambao wanacheza ugenini lakini kilichotokea kimewasikitisha.

Mabingwa watetezi wa Eredivisie Ajax,wanafundishwa na beki wa zamani wa Uholanzi Frank de Boer,na wanafanya safari kwenda huko Phillips Stadium mchezo utakaopigwa Jumapili.

Wanakamata nafasi ya 4 wakikusanya pointi 11 baada ya mechi 6 na watakaa juu ya PSV kama watapata ushindi Jumapili.

PSV ambao hawajapoteza mchezo wanakamata nafasi ya pili wakiwa na pointi 12 ikiwa ni pointi moja nyuma ya wanaoongoza ligi PEC Zwolle.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.