West Bromwic Albion wameitolea nje ofa ya kumuuza mshambuliaji wake Peter Osaze Odemwingine.
Mshambuliaji huyo anafanya mazoezi na wachezaji wanaosugua bench kufuatia mpango wake wa kulazimisha kutimkia QPR kwenye usajili wa dirisha dogo mwezi January.
Fulham wanaripotiwa kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo wa Nigeria kwa dau la paundi milioni 1.5 lakini boss wa West Brom Steve Clarke akizungumza mwezi May alisema thamani ya Odemwingie ni paundi milioni 4.5.
Dau hilo bado halimzuii kocha wa Fulham Martin Jol kumnasa mshambuliaji huyo kwa nusu ya fedha hizo.
Fulham sasa imenunuliwa na billionaire tycoon Shahid Khan,ambaye ameinunua klabu hiyo kutoka kwa Mohamed Al Fayed kwa dau la paundi milioni 150.
Mkataba wa Odemwingie huko West Brom unamalizika mwezi June mwakani.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.