Wednesday, July 31, 2013
Chelsea yahamia kwa Khedira
Real Madid kutumbukia kwa Gareth Bale kumeiamsha Chelsea na sasa inataka kuweka paundi milioni 20 kumnasa kiungo raia wa Ujerumani Sami Khedira.
Madrid wameweka dau la rekodi ya dunia la paundi milioni 85 na hilo linawafanya pia kutaka kutunisha mfuko wao kwa kuuza wachezaji jambo linalomfanya Mourinho kutaka kutumbukia kumnasa Khedira.
Mpango huo wa Mourinho unaweza kufanikiwa hasa baada ya kutua kwa kiungo kinda Asier Illarramendi na Isco.
Mourinho anataka kuimarisha kiungo kutokana na kiungo Frank Lampard kukaribia kutundika daruga,Michael Essien anasumbuliwa na maumivu na John Obi Mikel anaweza kuondoka.
Khedira mwenye miaka 26 alijiunga Madrid akitokea Stuttgart mwaka 2010 na amekuwa na mahusiano mazuri na Mourinho.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.