Wednesday, July 24, 2013

Ashanti waiendea Yanga Burundi

Wauza mitumba wa Ilala Ashanti United wameondoka kuelekea mkoani Kigoma na baadaye nchini Burundi kwa maandalizi ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu ujao.

Rais wa Ashanti Alhaj Ahmed Msafiri Mgoyi amethibitisha timu hiyo kuondoka kwa kambi hiyo ya mwezi mzima ambayo itaishia nchini Burundi watakapocheza mechi 2 au 3 za kirafiki.

Alhaj Mgoyi amesema kwasasa mawasiliano yanaendelea na shirikisho la kabumbu hapa nchini TFF kuhusiana na safari hiyo ya Burundi ili kuweza kufanikisha lengo lao.

Amesema taratibu nyingine zinaendelea ikiwa pamoja na kuomba kibali kwa TFF cha kutoka nje ya Tanzania.


Ashanti United imepanda tena daraja na wameahidi kufanya makubwa katika msimu ujao unaotaraji kuanza kuunguruma August 24 kwa wakali hao kufungua pazia dhidi ya bingwa mtetezi Yanga Africa.



No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.