Kiungo wa Barcelona Cesc Fabregas bado ni habari ya mujini,wakati Manchester United ikitumbukiza dau la paundi milioni 25 kutaka kumsajili,mwenyewe amesema hataki kuondoka Nou Camp.
Kocha wa Barcelona Tito Vilanova amesema kuwa licha ya Man U kugonga hodi kuhitaji huduma yake lakini mwenyewe ametamka kuwa anataka kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo.
Nikiondoka hapa si ndio mataji nayo yanaota mbawa...
Vilanova anasema amezungumza na Fabregas na amemwambia wazi kuwa ndoto yake ni kuendelea kubaki kwenye klabu hiyo na hana sababu ya kwenda klabu nyingine kwasababu ya fedha au kwasababu ya kupata muda wa kucheza zaidi uwanjani na anafahamu kuna ushindani wa namba ndani ya klabu hiyo lakini anataka kubaki na kupigania namba.
.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.