Monday, July 22, 2013

Libolo tishio,Samatta akifanya yake Africa


Timu ya Recreativo de Libolo ya Angola imeendelea kutisha kwenye ligi ya mabingwa barani Africa ikiutumia vizuri uwanja wake wa nyumbani wa Municipal de Calulo.

Bao la dakika ya 94 likiwekwa wavuni na Aguinaldo limetosha kuwaweka kwenye nafasi nzuri kwenye mchezo waliocheza dhidi ya Esperance de Tunis katika mchezo wa kundi B.

Ni mwanzo mzuri kwa Libolo ambao wanacheza kwa mara ya kwanza hatua hiyo ya makundi ya ligi ya mabingwa.

Libolo iliwaondoa Al-Merreikh na Enugu Rangers ya Nigeria kuifikia hatua hiyo ya makundi kwa mara ya kwanza kwenye historia yao.

     Nipishe dogo...


Huko kwenye kombe la shirikisho Tp Mazembe ya Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo bao la Mbwana Samatta Popa liliisaidia timu hiyo kupata sare ya bao 1-1 dhidi ya Etente Setif ya Algeria.

Nazo FUS Rabat ya Morocco na CA Bizertin ya Tunisia zimetoka sare ya kufungana bao 1-1

Katika kundi A Saint George ya Ethiopia imepata ushindi wa mabao 2-0 mbele ya Stade Malien ya Mali mchezo uliochezwa Addis Ababa.

Mabao ya St George yamewekwa wavuni na Omod Okury na Gebremariam.


Wakati huo huo wakati wa wikiendi ilishuhudiwa Orlando Pirates ya Africa kusini ikilazimishwa suluhu ya bila kufungana na AC Leopards ya Congo Brazzaville kwenye ligi ya mabingwa.

No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.