Saturday, July 13, 2013

Moyes akaribishwa Man U kwa kichapo

Kocha mpya wa Manchester United David Moyes amekaribishwa rasmi kwenye timu hiyo kwa kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Singha All Stars huko Thailand.

Teeratep Winothai alifunga katika dakika ya 50 katika mchezo huo uliopigwa Rajamangala National Stadium ndani ya Bangkok.
     Nyie watoto hamjui kama siye ni wakubwa alaaa..

Kwenye mchezo huo kinda Wilfried Zaha,aliyesajiliwa kutoka Crystal Palace na kinda mwingine mwenye miaka 18 Adnan Januzaj wote walipata nafasi ya kuichezea timu hiyo kwa mara yao ya kwanza na walikosa kosa kuzifumania nyavu mara kadhaa.


Kufuatia kutokuwepo kwa Wayne Rooney ambaye amerejea England kwaajili ya kupata matibabu,kukosekana kwa Javier Hernandez, Robin van Persie na Nani,ilikuwa ni nafasi ya vijana kuonyesha njaa yao.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.