Taarifa zinasema kuwa mshambuliaji Wayne Rooney yupo karibu kutua Chelsea inayotaka kumpa mshahara wa paundi laki 2 kwa wiki,huku akitamka kuwa anataka kuungana na Mourinho.
Chelsea wanataka kupandisha dau lao la kumnasa Rooney kufikia paundi milioni 40 ikiwa ni ofa kubwa zaidi ya ile waliyoanza nayo inayokadiriwa kufikia paundi milioni 25 ambayo ilichomolewa na Manchester United.
Kuna matumaini makubwa kwa Chelsea kumsajili mshambuliaji huyo ambaye hatamani kuendelea kuwepo United na matakwa yake ni kutua Chelsea kuungana na kocha Jose Mourinho ambaye tayari amesema atamfanya mshambuliaji huyo kuwa chaguo la kwanza na atamfanya kuwa Special one kama alivyo yeye.
Kocha wa United David Moyes na makamu mwenyekiti Ed Woodward,wameendelea kusema Rooney hauzwi lakini Chelsea wanaendelea kukomaa kuona mwisho wake.
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.