Wednesday, July 17, 2013

Simba yabariki rungu la TFF kwa Kazimoto

Wekundu wa Msimbazi Simba wamebariki kiungo wake Mwinyi Kazimoto Mutula kuadhibiwa na shirikisho la soka nchini TFF baada ya kutoroka kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Starz.

Afisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga amesema kitendo alichofanya Kazimoto hakikubaliki na kimekwenda kinyume na maadili ya mchezaji na kinyume cha maadili ya kambi ya Taifa Starz.

Kamati ya utendaji ya Simba itakutana na kujadili hatua hiyo ya Kazimoto kutorokea Qatar kwenda kusaka timu ya kucheza bila ya ruhusa kutoka TFF na uongozi wa Simba.

Kamwaga amesema kazimoto hawezi kucheza kokote bila ruhusa ya Simba na kamati ya utendaji baada ya kumjadili itatoa tamko la kile kilichojadiliwa.

Tayari shirikisho la soka nchini TFF limesema kuwa litamuadhibu kiungo huyo kwa kuwa amekwenda tofauti na kanuni alizosaini za kambi ya Taifa Starz.


No comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.