Sunday, July 14, 2013
Man U wamepigwa bao la mwaka
Mashetani Wekundu wa Manchester United wamepigwa bao la mwaka baada ya Bayern Munich kumaliza utata na itamsainisha kinda wa Barcelona aliyekuwa ananyatiwa pia na mashetani hao Thiago Alcantara kwa dau la paundi milioni 21.
Kiungo huyo wa Hispania mwenye miaka 22,anakwenda kuungana na kocha wa zamani wa Barca Pep Guardiola aliyeanza kumtumia wakati akiwa na miaka 18.
Sasa nazungumza kama captain,sijui mnanielewa..
Mwenyekiti wa Bayern Karl-Heinz Rummenigge amesema Alcantara ni matakwa na chaguo la kocha Pep Guardiola.
Mabingwa hao wa Ujerumani wamesema kinda huyo atamalizana na vipimo vya afya huko Munich kabla ya kusaini mkataba wa miaka minne.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.